sw.news

Duka Kubwa La Kijerumani Lafutilia Mbali Misalaba

Duka kubwa la Kijerumani la Lidl lilichapisha tena kanisa maarufu la Anastasis la Santorini, Ugiriki, kwenye pakiti zake za menyu mpya ya vyakula vya Kigiriki, na kwa wakati huo huo, kufuta misalaba ya paa za samawati za kuba ambazo ni maarufu duniani kote.

Lidl walieleza katika mataifa kadhaa kuwa uamuzi huu uliafikiwa ili kuheshimu "utofauti", madai ambayo yanasingizia kuhusisha aina tofauti ya watu, vikundi au mashirika lakini ni kana kwamba ukweli unawaepua Wakristo.

Tawi la duka la Lidl nchini Australia ndilo la pekee kuomba msamaha kwa walichokiita "makosa".

Kadinali Dominik Duka wa Prague, Taifa la Czech, siku ya Jumatatu aliita jambo hili katika barua kwa Ubalozi wa Ugiriki, "kitendo chs ujeuri na kisicho na mila". Duka anahofia kuwa hatua itakayofuatia ni kuwa hatimaye misalaba itaondolewa kwenye Makanisa halisi.

#newsOjjievhpot
118